KANUNI ZA KIBIBLIA ZA USIMAMIZI WA FEDHA





“kanuni za kibiblia za usimamizi wa fedha zitakazo linda na kustawisha uchumi wako”

UTANGULIZI:
Kuna mafundisho mengi kuhusu jinsi ya kufanya biashara,kufanya ujasiriamali,kufanya miradi ,Kujiari n.k yote yaki lenga katika kuzalisha na kupata fedha au kukuza uchumi.lakini kuna mafundisho kidogo kuhusu upande wa pili ambao ni wa muhimu sana katika uchumi,jinsi ya kusimamia fedha.matatizo makubwa ni namna ya kusimamia fedha kuliko jinsi ya kuzalisha fedha.
wengi tuna pata fedha tatizo ni jinsi ya kuzisimamia,somo  hili litazungumzia eneo hili la pili la “ jinsi ya kutumia kanuni za kibiblia za usimamizi wa fedha ili kuulinda na kustawisha uchumi wetu.”


                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                       
KANUNI KUMI ZA KIBIBLIA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA:
Biblia inatoa mwongozo mzuri wa usimamizi wa fedha ambao tukiufanyia kazi tuta punguza kwa asilimia kubwa matatizo mengi ya kifedha tuliyo nayo.Matatizo mengi ya kifedha tuliyo nayo yanachangiwa sana kwa namna moja au nyingine na usimimamizi mbaya wa fedha zetu,wengi wetu tatizo letu kubwa zaidi ni usimamizi wa fedha kuliko kuzalisha na kupata fedha.

usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako na kuukuza uzalishaji wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini kama una usimamzi mbaya wa fedha  uchumi wako utayumba tu.Matatizo mengi ya kifedha tunakimbilia kuombewa na kukemea,lakini hayo yote bila  kujifunza usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika mzizi.hata ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha matatizo ya kifedha yatarudi baada ya muda mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi kanuni za fedha.

1.       MUNGU NDIYE MMILIKI WA FEDHA ZETU
Fedha ni Mali ya Bwana,sisi tu wasimamizi tu au mawakili,hivyo tunawajibika na vile tunatumia kila fedha tuliyoaminiwa na Mungu.( Mathayo 25:1-30 ; Zaburi 24:1,)

2.       TAMBUA FEDHA NI SUALA LA KIROHO.
Kwa mtu wa Mungu fedha ni suala la kiroho,fedha ina athiri na inagusa maisha yako ya kiroho pia.vile unavyo shughulika na fedha kuna sema zaidi juu ya hali yako ya moyo kuliko ushuhuda wako.vile unavyoshughulika na fedha zako ni kiashirio cha ukomavu wako kiriho.LUKA 16:10-11
Fedha inaweza kuwa mungu wako,fedha ina uwezo zaidi kutuvuta taratibu na kwa ujanja kutoka kwa Mungu kuliko kitu kingine chochote.MATH 6:24,Ina nguvu ya kuwa Bwana wetu.
Katika mifano 38 ya Yesu,16 inahusu fedha,katika agano jipya fedha imezungumzwa zaidi kuliko habari za mbinguni na kuzimu vikiunganishwa pamoja.mara tano zaidi imezungumzwa kuhusu fedha kuliko maombi,kuna mistari zaidi ya 1500 inayohusu maombi na imani,wakati kuna zaidi ya mistari 2000 inayohusu fedha na mali.Aslimia 15% ya Biblia  ni kuhusu fedha.

3.       TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA
Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza kukusaidia katika kuandaa bajeti yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari ndogo na anza kuweka kumbukumbu za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini itakusaidi kwa mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa usafiri?simu?chakula?matibabu?chakula n.k ni lazima ujue wapi fedha yako inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina mililki,nini nina dai,nini nina daiwa,natuamiaje(MITHALI 27:23-24, 23:23,)

4.       FANYA TATHIMINI  YA MARA KWA MARA YA FEDHA ZAKO:
ni muhimu kufanya tathimini kwa uaminifu kuhusu uchumi wako,mapato yako,madeni,vitega uchumi vyako n.k. hii itakusadia kufanya marekebisho unayoyahitaji na  kukusaidia kuishi kwa mpango,kama huwezi kutathimini hutaweza kupanga,ukishindwa kupanga,tayari umeshindwa kusimamia fedha yako.(MITHALI 21:5  LUKA 14:28)

5.       JIWEKEE  MFUMO WA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA:
Bajeti kirahisi nikuandika  katika karatasi nini unategemea kupata kama mapato na njisi gani unategemea kutumia.panga matumizi yako.Ni mpango wa jinsi gani utatumia rasilimali  fedha ambazo unatarajia kupata ,bajeti inapaswa ijumuishi vyanzo vya mapato  pia mpango wa matumizi wa mapato mf.mpango wa chakula,kodi,zaka,utoaji,akiba n.k(Mithali 21:5, Mithali 21:20)

6.       JIWEKEE  UTARATIBU WA KUWEKA AKIBA
Weka Akiba, kwaajili ya dharura,akiba kwaajili malengo maalumu, (Mithali 21:20a ;13:11)
Mithali 6. Tenga kiasi cha kuweka akiba anza na kiasi kidogo kwanza.

7.       JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU-
(Mithali 11:24-25).kanuni ya uchumi wa Kimungu ni tofauti,kadiri unavyotoa na sivyo unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa kwaajili ya kuwabariki wengine,kutoa kwaajili ya wahitaji(Mithali 28:27 Mithali 11:25.Mithali 19:17,Mithali 3:9-10),Kutoa  kunafungua Baraka za Mungu katika Maisha yako.

8.       TUMIA FEDHA YAKO KWA HEKIMA NA RIDHIKA NA ULICHO NACHO:
Zingatia vipaumbele na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila mpangilio,manunuzi ya papo kwa papo,usifanye matumizi yaliyo nje,yanayozidi kipato chako au uwezo wako wa kifedha.Jifunze kuridhika na kuuepuka tamaa.usifuje fedha kwa matumizi ya ovyo.jifunze kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9) 

9.       TUNZA VITU NA MALI AMBAVYO UMEVIGHARIMIA FEDHA.
Vitu,mali ni fedha,usipovitunza utatoa fedha tena kununua. Tunza visiharibike ovyo,vitumike kwa uangalifu ili kuokoa gharama ya matengenezo au kununua upya.

10.   EPUKA MADENI.
biblia haijakataza moja kwa moja kuhusu kukopa,ila kwa uwiano wa maandiko Haiti moyo madeni,bali inakatisha tamaa kukopa.inazungumza zaidi madhara ya kukopa.Unapokuwa katika deni unakuwa katika kifungo,Madeni yana haribu uhusiano.usitumie fedha zaidi ya ile unayozalisha utaishia kwenye madeni.weka akiba kidogo kidogo badala ya kukopa.
MITHALI 22:26-27,ZABURI 37:21,MITHALI 22:7

HITIMISHO:
Pengine umekuwa unapitia katika kipindi kigumu cha kifedha,uchumi wako umeyumba,kabla ya kuhitaji fedha zaidi unahitaji kuzifanyia kazi kanuni hizi za usimamizi wa fedha.Mungu anakusubiri ujifunze na kuzingita kanuni hizi za fedha ili akufungulie mlango mkubwa zaidi wa kifedha,ni jukumu lako kutii kanuni hizi na hali yako ibadilike au ubaki katika hali uliyo nayo.Mungu akubaliki unapochukua uamuzi wa kusimamia fedha zako kama wakili mwaminifu.MUNGU akubariki sana . By pastor Mtitu.

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More